Rahisisha usimamizi wa hati ukitumia iLovePDF Business

Suluhisho zenye ufanisi, kuaminika na salama kwa PDF zako zote – wezesha biashara yako kwa ujumuishaji rahisi wa PDF na zana za ushirikiano.

Wasiliana na idara ya mauzo
Biashara Biashara

Inaaminiwa na makampuni mashuhuri

burberry dior hp linkedin nh philips nestle luxotica oracle samsung toyota starbucks accion europastry galicia lefosse manpower
burberry dior hp linkedin nh philips nestle luxotica oracle samsung toyota starbucks accion europastry galicia lefosse manpower

Imepewa ukadiriaji wa juu kwa kuwa na kiolesura rafiki kwa mtumiaji na zana za PDF zenye matumizi mengi

Wateja wanaiamini iLovePDF kama suluhisho la kuaminika, linalofaa kwa kusimamia mitiririko changamano ya biashara kwa urahisi

Bora zaidi kwa urahisi wa kutumia
Bora zaidi kwa urahisi wa kutumia
Zana rahisi zinazoendana kikamilifu na mitiririko ya kazi za biashara yako.
Capterra, 2026
Inayopendekezwa zaidi
Inayopendekezwa zaidi
Inapendekezwa na timu zinazobadilisha hati kuwa za kidijitali kila siku.
Software Advice, 2026.
Thamani bora zaidi
Thamani bora zaidi
Utambuzi mahiri wa maandishi unaokuwezesha kupata manufaa zaidi kutoka kwa kila ukurasa.
Capterra, 2026
Watumiaji
Watumiaji wanatupenda
Zana za PDF ambazo timu hurudia kutumia, siku baada ya siku.
G2, 2026

Jukwaa lako la kazi zote katika sehemu moja kwa mahitaji yako yote ya hati

Zana

Jukwaa moja la kufanya kazi kwa urahisi

Badilisha na Punguza Ukubwa: Badilisha PDF kwenda na kutoka katika aina mbalimbali za faili (Word, Excel, PowerPoint) na punguza ukubwa wa faili bila kupoteza ubora.

Hariri na Onyesha Maelezo: Ongeza maandishi, picha, maelezo ya ziada, na taswira fifi. Unganisha, gawa, na panga upya kurasa ili kuandaa hati kulingana na mahitaji yako.

Saini Kielektroniki: Saini nyaraka kwa njia ya kidijitali na omba saini kutoka kwa wengine, hivyo kurahisisha michakato yako ya idhini.

Rahisi

Kuboresha tija ya biashara yako

Rahisi kutumia: Vinjari kwa urahisi kwenye kiolesura kilicho safi na rahisi kueleweka kilichoundwa kwa ajili ya urahisi na ufanisi wa kazi.

Fanya kazi kutoka kwenye kifaa chochote—ikiwa ni kompyuta, kishikwambi au simu. Hii inahakikisha kwamba timu yako inaweza kushughulikia PDF kwa urahisi, iwe wakiwa ofisini, nyumbani, au wakiwa safarini.

Miunganisho ya API: Unganisha na programu nyingine kama Odoo, ChatGPT na WordPress.

Saini ambazo timu yako inaweza kuziamini

Saini za Kielektroniki za Kiwango cha Juu (AES): Pata zaidi ya saini ya kawaida kwa utambulisho uliothibitishwa wa mtia saini na nyaraka zinazoonyesha dalili za mabadiliko yasiyoidhinishwa, kwa mikataba ambayo ushahidi ni muhimu.

Tayari kwa eIDAS: Imeundwa kwa kuzingatia kiwango cha Ulaya cha saini za kielektroniki, ili makubaliano yako yatambuliwe kote katika Umoja wa Ulaya.

Usalama

Usalama wa hati

Ulinzi wa Data wa Kiwango Bora: Linda hati zako kwa kutumia hatua za usalama wa hali ya juu, ikiwa ni pamoja na uthibitishaji wa vipengele vingi (MFA), mfumo wa kuingia mara moja (SSO) unaoruhusu watumiaji kuingia kwenye huduma nyingi kwa kutumia kitambulisho kimoja, na usimbaji wa data.

Uzingatiaji: Timiza viwango na kanuni za sekta, kwa kutumia vipengele vilivyoundwa kusaidia mahitaji ya uzingatiaji wa sheria.

SSO
SSO (Kuingia mara moja)
Njia moja salama ya kuingia kwa kila mtu, inayosimamiwa kupitia mtoa huduma wako wa utambulisho.
Uchakataji wa mkupuo
Maeneo ya uchakataji wa faili
Chagua mahali faili zako zinapochakatwa ili kukidhi mahitaji yako ya uzingatiaji wa kanuni.
Msimamizi Maalum wa Akaunti
Msimamizi Maalum wa Akaunti
Usaidizi unaokulenga binafsi kutoka kwa mtu anayeelewa jinsi timu yako inavyofanya kazi.
Mkataba maalum
Mkataba maalum
Masharti na taratibu za utozaji na ununuzi zinazoendana na jinsi kampuni yako inavyonunua.

Zana zaidi ya 30 za kushughulikia kazi za PDF

Hariri PDF
Badilisha PDF
OCR
Saini ya kieletroniki
Linganisha
Unganisha na Gawa

Hariri maandishi ya PDF

  • Badilisha moja kwa moja maandishi yaliyopo kwenye PDF, na kuondoa haja ya kubadilisha kwanza kwenye muundo mwingine ndipo ufanye marekebisho.
  • Sasisha au rekebisha taarifa kwa haraka na kwa ufanisi, huku ukihifadhi muda kwenye marekebisho ya nyaraka.
Hariri maandishi ya PDF

Badilisha PDF na Office

  • Geuza hati za PDF kwa urahisi kuwa muundo wa Microsoft Word, Excel, na PowerPoint na kinyume chake.
  • Rahisisha matumizi na uhariri wa hati kwa kubadilisha kwa urahisi kati ya miundo ya PDF na Office.
Badilisha PDF na Office

Utambuzi wa maandishi kwa kutumia OCR

  • Badili hati zilizochanganuliwa pamoja na picha kuwa maandishi yanayoweza kutafutwa na kuharirika, huku ukiboresha upatikanaji wa data.
  • Boresha ufikiaji wa hati kwa kubadilisha maandiko yaliyochapishwa au yaliyoandikwa kwa mkono kuwa maandiko yanayosomwa na mashine.
Utambuzi wa maandishi kwa kutumia OCR

Saini ya kieletroniki

  • Saini kidijitali hati za PDF, ili kufanya mchakato wa kutia saini kuwa wa haraka na rahisi zaidi.
  • Hakikisha uadilifu na uhalisi wa hati kwa kutumia saini za kielektroniki zilizo salama.
Saini ya kieletroniki

Ondoa taarifa nyeti na Linganisha PDF

  • Ondoa kabisa taarifa nyeti kutoka kwenye PDF ili kulinda faragha na usiri.
  • Tambua na angazia tofauti kati ya toleo mbili za PDF, ili kurahisisha ukaguzi wa nyaraka.
Ondoa taarifa nyeti na Linganisha PDF

Weka manukuu kwenye PDF

  • Weka maoni, alama, na michoro kwenye PDF, ili kurahisisha ushirikiano na mrejesho.
  • Tumia zana mbalimbali za vidokezo ili kuweka alama kwenye hati kwa ajili ya uwazi na mawasiliano yaliyoboreshwa.
Weka manukuu kwenye PDF

Unganisha na Gawa

  • Unganisha faili nyingi za PDF kuwa hati moja kwa ajili ya urahisi wa kupanga na kusimamia.
  • Gawa PDF kubwa kuwa faili ndogo, na kuifanya iwe rahisi kuzishughulikia na kuzisambaza.
Unganisha na Gawa

Kubadilisha mitiririko ya kazi ya hati ulimwenguni kote

25 bora

tovuti inayotembelewa zaidi duniani

16.5M

hati zinazochakatwa kila siku

Zaidi ya Elfu 20

biashara zinazotumia iLovePDF

4.9

kwenye Trustpilot

quote

"iLovePDF imeleta mapinduzi makubwa katika mchakato wetu wa usimamizi wa hati. Zana zake rahisi za kubadili, kubana na kuhariri faili zimeokoa muda mwingi sana na mfumo wake rahisi wa utumiaji unafanya iwe rahisi kwa kila mtu kwenye timu yetu kutumia. Sasa tunaweza kushughulikia mahitaji yetu yote ya hati mahali pamoja, jambo ambalo limeongeza ufanisi wa utendaji kazi wetu kwa kiasi kikubwa. Tunaipendekeza sana iLovePDF kwa biashara yoyote inayotaka kurahisisha majukumu yake ya hati kila siku!”

Tristan Lecrivain

Mkuu wa Idara ya Mauzo ya Kikanda wa Saab

Imeundwa kwa ajili ya kampuni ya biashara

Rahisisha michakato ya kazi
  • Chakata hati nyingi kwa mkupuo ili kuokoa muda na kuongeza ufanisi.
  • Jumuisha na Hifadhi ya Google na Dropbox kwa urahisi na kwa tija.
Boresha kazi kwa AI
  • Dondoa maandishi kwenye faili zilizochanganuiliwa ukitumia OCR inayotumia AI.
  • Fanya kazi kiotomatiki na boresha matokeo kwa kutumia zana zinazoendeshwa na AI.
Usalama wa kiwango cha biashara
  • Linda data kwa usimbaji fiche wa mwanzo hadi mwisho.
  • Tafsiri, fupisha na badilisha kuwa Markdown, yote kwa kutumia salio moja la krediti za AI
Msaada na seva maalum
  • Usaidizi maalum kutoka kwa meneja mahsusi.
  • Mipangilio maalum ya kiufundi kwa ajili ya biashara yako.
Usimamizi wa timu na ruhusa
  • Dhibiti majukumu na ruhusa kupitia dashibodi kuu.
  • Tuma nembo, kiolezo na vifaa vya chapa kwa uthabiti.
Fanya mtiririko wa kazi kiotomatiki kwa kutumia API
  • Ujumuishaji rahisi pamoja na mwongozo na mifano.
  • Fanya kiotomatiki kazi zilizoanzishwa na matukio ya nyaraka.

Gundua jinsi iLovePDF inavyorahisisha usimamizi wa nyaraka kwenye sekta yako ya biashara

Rasilimali Watu
Ya Kisheria
Fedha
Mali Isiyohamishika
Bima
Huduma za Afya

Rasilimali Watu

  • Usimamizi wa Nyaraka: Wataalamu wa Rasilimali Watu mara nyingi hushughulikia idadi kubwa ya nyaraka kama wasifu, mikataba, na kumbukumbu za wafanyakazi. iLovePDF hurahisisha kuunganisha, kugawa, na kuweka maelezo kwenye PDF, hivyo kurahisisha usimamizi wa nyaraka.
  • Sahihi za Kielektroniki: Kipengele cha e-Sign hurahisisha mchakato wa kuajiri kwa kuruhusu kusaini kwa haraka na kwa usalama mikataba ya ajira na hati nyingine zinazohusiana na rasilimali watu.
Rasilimali Watu

Sekta ya Sheria

  • Uondoaji na Ulinganishaji wa Taarifa Nyeti: Wanasheria mara nyingi hufanya kazi na taarifa nyeti. Zana za uondoaji wa taarifa nyeti za iLovePDF husaidia kuondoa kwa usalama data za siri, wakati kipengele cha kulinganisha husaidia kubaini mabadiliko kati ya matoleo tofauti ya hati za kisheria.
  • OCR na Uhariri wa Maandishi: Wataalamu wa sheria wanaweza kutumia OCR kubadilisha hati zilizoskaniwa kuwa maandishi yanayoweza kuhaririwa, na kurahisisha uhariri na utafutaji wa vipengele fulani kwenye maandiko makubwa ya kisheria.
Sekta ya Sheria

Huduma za Kifedha

  • Ubadilishaji na Uhifadhi: Wachambuzi wa masuala ya kifedha na wahasibu mara nyingi huhitaji kubadilisha ripoti na taarifa za kifedha kati ya PDF na Excel kwa ajili ya uchambuzi. Ubadilishaji kuwa PDF/A unahakikisha nyaraka hizi zinahifadhiwa katika umbizo linalokidhi masharti na linaloweza kufikiwa kwa urahisi.
  • Usalama na Usiri: Kipengele cha uondoaji wa taarifa nyeti kinahakikisha kwamba taarifa nyeti za kifedha zinaendelea kuwa za siri, na zana ya e-Sign inarahisisha kusaini mikataba ya kifedha kwa usalama.
Huduma za Kifedha

Mali Isiyohamishika

  • e-Sign na Udhibiti wa Hati: Madalali wa mali zisizohamishika wanaweza kuharakisha mchakato wa kusaini mikataba na makubaliano kwa kutumia kipengele cha e-Sign. Kuunganisha, kugawa, na kuweka maelezo kwenye PDF husaidia kusimamia hati za mali kwa ufanisi.
  • Uondoaji wa taarifa nyeti: Ondoa kwa usalama taarifa binafsi kutoka kwenye hati kabla ya kuzituma kwa wanunuzi au wapangaji watarajiwa, ili kuhakikisha utii wa sheria za faragha.
Mali Isiyohamishika

Bima

  • Uchakataji wa Madai na Polisi za Bima: Kampuni za bima hushughulikia mtiririko endelevu wa fomu za madai, nyaraka za polisi za bima na ushahidi wa kuunga mkono madai. OCR hubadilisha fomu zilizochanganuliwa na nyaraka zilizopigwa picha kuwa maandishi yanayoweza kutafutwa, huku kuunganisha na kugawanya kukisaidia kuweka kila faili la dai katika mpangilio kuanzia taarifa ya kwanza hadi utatuzi wa dai.
  • Kutia Saini Kielektroniki na Usiri: Kipengele cha kutia saini kielektroniki huharakisha uhuishaji wa polisi za bima na utatuzi wa madai kwa kuwezesha utiaji saini salama wa kielektroniki. Ufichaji wa taarifa nyeti huondoa data binafsi na za matibabu kabla ya faili kushirikiwa na madalali, wakadiriaji wa madai au wahusika wengine, hivyo kusaidia kuzingatia kanuni za faragha.
Bima

Huduma za Afya

  • Usimamizi wa Rekodi za Wagonjwa: Wataalamu wa afya hushughulikia kiasi kikubwa cha data za wagonjwa, kuanzia historia za matibabu hadi matokeo ya maabara. iLovePDF inarahisisha kuunganisha, kugawa, na kupanga hati ili kudumisha rekodi sahihi na za kisasa.
  • Usalama wa Data na Uzingatiaji wa Sheria: Zana za kuficha taarifa za iLovePDF husaidia kuondoa kwa usalama taarifa nyeti za wagonjwa kutoka kwenye nyaraka kabla ya kuzishiriki, na hivyo kuhakikisha uzingatiaji wa kanuni za faragha za huduma za afya kama HIPAA.
Huduma za Afya

Washirika wetu wa teknolojia

Uhariri wa Kina wa PDF
Google Workspace
Ingiza na hamisha faili moja kwa moja kwenye Hifadhi ya Google, ili kurahisisha usimamizi wa hati zako ndani ya Google Workspace.
Uhariri wa Kina wa PDF
Dropbox
Pata na hifadhi faili zako za PDF kwa urahisi kutoka na kwenda Dropbox, ukihakikisha nyaraka zako ziko sawa kila wakati kwenye vifaa vyote.
Uhariri wa Kina wa PDF
Auth0
Unganisha na ujumuishaji wetu wa SSO, ukitoa ufikiaji salama kwa kuruhusu wafanyakazi kutumia seti moja ya vitambulisho kwenye zana mbalimbali za kampuni.
Uhariri wa Kina wa PDF
Zapier
Fanya mtiririko wako wa PDF kiotomatiki kwa kuunganisha iLovePDF na maelfu ya programu nyingine kupitia Zapier, na kuwezesha uwekaji kiotomatiki maalum bila kuandika msimbo wowote.
Uhariri wa Kina wa PDF
WordPress
Weka programu jalizi kwenye WordPress kwa upachikaji na utumaji rahisi wa PDF kwenye tovuti yako, ili kuboresha usimamizi na uwasilishaji wa maudhui.
Uhariri wa Kina wa PDF
Power Automate
Unganisha iLovePDF na programu za Microsoft ili kurahisisha kazi za PDF kama kubadilisha fomati, kupunguza ukubwa, na kusaini—vyote bila juhudi zako mwenyewe.

Hati zako zinastahili ulinzi bora zaidi

Usalama

Jifunze jinsi tunavyoipa faragha na usalama wa data yako kuwa kipaumbele chetu




Pata maelezo zaidi

Anza kutumia iLovePDF leo

macOS
Inatumia macOS 12 au toleo la baadaye
macOS
Windows
Inatumia Windows 10 au toleo la baadaye
Microsoft Store
iOS
Inatumia iOS 18.6 au toleo la baadaye
iOS
Android
Inatumia Android 8.0 au toleo la baadaye
Android

Tutafute mpango unaofaa timu yako

Jukwaa moja kwa kila mtiririko wa kazi za PDF katika shirika lako, lenye usalama, chaguo za usakinishaji na masharti ya ununuzi ambayo timu za makampuni makubwa zinahitaji.

  • Bei za ununuzi wa wingi zinazoendana na idadi ya wafanyakazi wako
  • Chagua kutumia kwenye wavuti, simu au kompyuta
  • SSO, mikataba iliyoundwa kulingana na mahitaji yako & msimamizi maalumu wa akaunti yako

Inaaminiwa na maelfu ya makampuni.


Kwa kutuma, unakubali Sera ya Faragha na Masharti ya Huduma ya iLovePDF

  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu iLovePDF Business
Lo! Kuna tatizo na muunganisho wako wa Intaneti...